Kocha wa zamani wa Simba, Milovan
Cirkovic amepata kazi mpya ya kuwanoa vijana.
Milovan raia wa Serbia amesema amepata
kazi ya kuwanoa wachezaji vijana katika klabu moja nchini humo.
“Ninaaanza kazi ndani ya siku mbili
hizi, baada ya hapo nitakuambia ni klabu gani lakini nimeshaini mkataba,”
alisema Milovan.
Milovan raia wa Serbia alikuwa kipenzi
cha Wanasimba lakini akaondoka baada ya kuona uongozi haumtaki.
Uongozi wa Simba ulimcheleweshea malipo
hadi alipojitokeza Malkia wa Nyuki na kuamua kumlipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment