Nahodha wa timu ya taifa ya Burundi, Kaze Gilbert
atasaini leo kuichezea Simba.
Tayari Kaze maarufu kama Demunga yupo jijini Dar es
Salaam na ameishakubaliana na Simba kuhusiana na maslahi na kilichobaki ni
kusaini tu.
“Kweli anasaini leo mchana na kila kitu
kimeishamalizika na yeye amekubali kusaini,” kilieleza chanzo.
Beki huyo wa kati wa Vital’O ambao ni mabingwa wa
Afrika Mashariki na Kati, alitua nchini juzi na jana alifanya mazungumzo na
uongozi wa Simba na kumalizana nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment