DEMUNGA AKIWA KAZINI |
Demunga ambaye ni beki kitasa wa mabingwa wa Kombe la Kagame, Vital’O na Inhamba Murugamba, ameishaanza mazungumzo na SImba na huenda akaja nchini kusaini mkataba.
Demunga amekuwa gumzo kati ya mabeki waliofanya vizuri katika michuano ya Kagame iliyofanyika nchini Sudan.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kwa asilimia 90 ni kama tayari ameishatua katika klabu hiyo.
Kama itafanikiwa kumnasa, maana yake Simba itakuwa na manahodha wawili kutoka nchini Burundi.
Ilianza kumnasa mshambuliaji Amisi Tambwe ambaye ni nahodha wa Vital’O iliyotwaa Kombe la Kagame na akaibuka mfungaji bora na mchezaji bora wa michuano hiyo iliyofanyika Sudan.
0 COMMENTS:
Post a Comment