Uongozi wa
Yanga umetumia wanasheria wanne kuwasilisha rufaa ya kupinga kufungiwa kwa
mshambuliaji Mrisho Ngassa.
Pamoja na
kupinga kufungiwa mechi sita, Yanga imepinga pia suala la Ngassa kutakiwa
kulipa Simba Sh milioni 45, ikiwa ni ziada ya Sh milioni 15 katika Sh milioni
30 anazodaiwa kuchukua alipoingia mkataba huo.
Msemaji wa
Yanga, Baraka Kizuguto amesema uamuzi huo umetokana na wao kushindwa kuelewa
utozwaji wa adhabu hizo.
“Tayari
tumewasilisha rufaa hiyo katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF
na wanasheria wanne kwa upande wetu wanalisimamia suala hilo,” alisema.
Kamati hiyo
chini ya Alex Mngongolwa ndiyo iliyotoa adhabu hizo na Ngassa anatakiwa kukosa
mechi sita za mashindano, ya kwanza ikiwa ni dhidi ya Azam FC ambayo Yanga
ilishinda na kutwaa Ngao ya Jamii.
Simba
ilitangaza kumuongezea Ngassa mkataba wa mwaka mmoja na ikampa gari pamoja na
Sh milioni 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment