Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, anatarajiwa kutupwa nje ya
uwanja kwa siku tatu kwa ajili ya kuuguza maumivu ya misuli ya paja.
Yondani alipata majeraha hayo katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi
ya Azam FC baada ya kugongana na kipa wake, Ali Mustapha ‘Barthez’ katika dakika
ya 18.
Daktari Mkuu wa Yanga, Nassor Matuzya, ameliambia Championi
Jumatatu kuwa, beki huyo atarejea uwanjani baada ya siku tatu kuanzia leo.
Matuzya alisema beki huyo anaendelea na matibabu yake vizuri,
hivyo mashabiki waondoe hofu katika mechi ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Ashanti,
kwani huenda akawepo uwanjani.
“Yondani alishindwa kumalizia mechi na Azam baada ya kugongana na
Barthez kwenye msuli wa paja lake wakati anajiandaa kuokoa mpira golini. Anatarajiwa
kurejea uwanjani baada ya siku tatu, ikiwa na maana ni Jumatano,” alisema
Matuzya.
0 COMMENTS:
Post a Comment