Beki kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, ameshonwa nyuzi moja mdomoni
baada ya kuchanika kutokana na kugongana na mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence
Mwaikimba.
Nyota huyo raia wa DR Congo, aligongana na mshambuliaji huyo
wakati timu hizo zilipocheza mechi ya Ngao ya Jamii juzi kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na Yanga kushinda bao 1-0.
Daktari Mkuu wa Yanga, Nassor
Matuzya, alisema kuwa beki huyo baada ya kuchanika mdomoni, damu zilimtoka
kabla ya kumshona.
Matuzya alisema beki huyo anaendelea vizuri na anatarajiwa
kuendelea na mazoezi ya pamoja na wenzake katika kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania
Bara.
“Mbuyu nilimshona nyuzi moja mdomoni mwake baada ya kugongana na
Mwaikimba wakati anajiandaa kuokoa mpira.
“Nilimshona muda uleule wakati mpira unaendelea kabla ya kuingia
kumalizia dakika zilizobakia za mechi hiyo, hivi sasa anaendelea vizuri na
ataendelea na mazoezi kujiandaa na ligi kuu,” alisema Matuzya.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment