Kipa namba moja wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’, amesema mshambuliaji
wa Azam FC, John Bocco, alidhamiria kumkanyaga tumboni kwa makusudi.
Barthez alikanyangwa na Bocco katika dakika ya 20 ya mchezo kati
ya timu hizo kuwania Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, juzi.
Alishindwa kuendelea na mchezo.
Barthez amesema kuwa mshambuliaji huyo hakuwa na nia ya kuucheza
mpira, badala yake alitaka kumuumiza kwa makusudi.
Barthez alisema amejifunza kupitia kwa mshambuliaji huyo, hivyo
ataongeza umakini kwa kucheza kwa tahadhari ili asipate tena majeraha kama
hayo.
“Kiukweli kabisa Bocco amenichezea rafu kwa makusudi kwa
kunikanyaga tumboni, inaonekana alidhamiria kufanya hivyo, kitu ambacho ni
kibaya, angalia jinsi alivyonisababishia uvimbe tumboni.
“Nimesikitishwa na kitendo hicho, lakini nimejifunza kwa hili
katika kukabiliana na washambuliaji wa aina hiyo,” alisema Barthez.
mwisho
0 COMMENTS:
Post a Comment