Wiki chache zilizopita baada ya kusaini mkataba wa mamilioni na Real Madrid na kuwa mwanasoka ghali zaidi duniani, Gareth Bale anatarajia kubeba mamilioni tena.
Kampuni kubwa ya mavazi duniani ya Adidas intarajia kumsainisha Bale mkataba mpya wa mamilioni ya pauni ingawa haijawekwa wazi.
Uongozi wa Adidas umethibitisha nia yake ya kutaka kumbakiza Bale na kumpa mkataba mpya ili achuane na Cristiano Ronaldo ambaye anadhaminiwa na Nike.
Adidas imekuwa ikimtumia Lionel Messi kuchukua na Ronaldo, lakini sasa inaonekana mkataba umesogea ndani.
Hii inakuwa sawa na ile ya Barcelona ilipomsajili Neymar mwenye mkataba na Nike, akawa anachuana ndani ya timu na Messi mwenye mkataba na Adidas.
0 COMMENTS:
Post a Comment