Katibu Mkuu Yanga, Lawrence Mwalusako
ameamua kuachia ngazi baada ya kukaimu kwa mwaka mmoja.
Mwalusako amesema amefanya hivyo kwa
kuwa makubaliano yao yalilikuwa ni kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.
“Haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu na
sasa muda mwafaka umefika wa kufanya hivyo,” alisema hivi punde.
Lakini uchunguzi wa Blog hii umeonyesha
kuwa Yanga imeleta Mkenya kuchukua nafasi yake hiyo na tayari ameanza kazi.
Mkenya huyo anajulikana kwa jina Patrick
Naggi kuchukua nafasi hyo.
Taarifa hizo zinaaleza Naggi amewahi
kuwa Technical Director wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) na CEO wa Tusker
ya Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment