Kumeibuka
maswali lukuki kuhusiana na Liverpool na uamuzi wao wa kumuuza kiungo mwenye ‘kipara’,
Jonjo Shelvey ambaye usiku wa jana alikuwa gumzo.
Shelvey
alikuwa gumzo wakati Liverpool ilipocheza dhidi ya Swansea katika mechi ya Ligi
Kuu England na kutoka sare ya mabao 2-2.
Ingawa
Liverpool imekaa kileleni lakini Shelvey amezua gumzo kubwa kutokana na kiwango
alichokionyesha na kuhusika katika mabao
yote manne ya mechi hiyo.
Shelvey
alitoa maboko mawili yaliyoipa Liverpool mabao lakini akafunga bao moja la
Swansea na kutoa pasi ya la pili lililofungwa na Michu.
Kuhusiana
na kiwango alionyesha kiwango cha juu na kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha
timu yake.
Liverpool
ilimuuza kiungo huyo kwa Swansea na wengi wameanza kuhoji kuhusiana na kuachwa
kwake.
0 COMMENTS:
Post a Comment