September 16, 2013

Liverpool imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea katika mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika hivi punde. 
Sare hiyo imeifanya Liverpool ipae hadi kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 10, Arsenal wanafuatia wakiwa na pointi 9.

Mechi hiyo ilikuwa tamu na ya kuvutia kutokana na mchezo kuwa wa kuvutia na ufundi mwingi kutoka kila upande.

Wenyeji Swansea ndiyo waliuanza mchezo kwa kasi na kupata bao katika dakika ya 2 mfungaji akiwa kiungo wa zamani wa Liverpool, Jonjo Shelvey.

Lakini Liverpool walisawazisha dakika mbili baadaye kupitia Danny Sturridge aliyejiunga na timu hiyo akitokea Chelsea.
Baada ya bao hilo, Liverpool waliendelea kuwa ‘tatizo’ kwa Swansea wakishambulia zaidi kwa mipira mirefu, hata hivyo mabeki wa timu hiyo walikuwa makini kuokoa.

Victor Moses aliifungia Liverpool bao la pili katika dakika ya 87 ambalo lilifanya matokeo yawe 2-1 hadi mapumziko.

Mwanzo wa kipindi cha pili, mambo yalibadilika na Swansea ndiyo walionekana kuutawala mchezo na kuipa Liverpool wakati mgumu hadi Michu alipofunga bao la kusawazisha katika dakika ya 63 baada ya kupokea pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Shelvey.

Baada ya hapo, Liverpool waliendelea kuwa katika wakati mgumu kutokana na mashambulizi mfululizo ya Swansea waliokuwa wamepania kupata ushindi wa kwanza msimu huu.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic