Mcheza
kriketi maarufu wa zamani wa Zimbabwe, alijikuta amelala chumba na mambo usiku
kucha bila ya kujua.
Guy
Whittall ,40, aliyekuwa nyota we mchezo huo nchini Zimbabwe alilala na mambo
huyo katika hoteli inayojulikana kama Humani Lodge.
Mambo
huyo mwenye kilo takribani 150 alikuwa chini ya kitanda chake akiuchapa
usingizi sawa na Whittall aliyekuwa kitandani akichapa usingizi.
Hakukuwa
na umbali mkubwa kutoka uso wa Whittall na mamba huyo na wote ‘walienjoy’ usingizi
usiku kucha.
Asubuhi,
Whittall aliinuka na kwenda jikoni kuandaa kifungua kinywa, lakini ghafla
alisikia kelele za dada aliyekuwa anafanya usafi ambaye alimuona mamba huyo
asili yake kutoka Mto Nile akiwa anaendelea kuuchapa usingiza.
Baada
ya hapo juhudi za kuanza kumtoa chini ya uvungu zilianza kupitia maofisa
wanyamapori ambao wananawasimia mbuga hizo, walifanikiwa kumkamata na
kumrudisha mbugani.
Hoteli
ya Humani Lodge iko katika eneo la moja ya mbuga za wanyama nchini Zimbabwe. Baadaye
mambo huyo alikamatwa na kurudishwa kwenye bwawa.
Akizungumzia
suala hilo, Whittall alisema: “Hauwezi kutegemea mambo kuamua kujificha chini
ya uvungu, hakika Mungu ameniokoa ila natoa ushauri kabla ya kwenda kulala kila
mtu akague chini ya uvungu wa kitanda chake, hauwezi kujua.”
Fin.
0 COMMENTS:
Post a Comment