September 19, 2013


Mwanariadha nyota, Usain Bolt amempa ujumbe Kocha Mkuu wa Manchester United, David Moyes kwamba ampunguzie presha.

Bolt mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani amemueleza Moyes kwamba huwa yuko katika hali ya wasiwasi sana kila Man United inapocheza.


Mwanariadha huyo wa Jamaica anaamini hali yake huwa mbaya zaidi kama timu hiyo inashindwa kucheza vizuri.

Bolt ametangaza atastaafu baada ya Michezo ya Olympiki. Anaendelea kushikilia rekodi ya sekunde 9.4 katika Mita 100.

Mjamaica huyo alisema alikuwa akivutiwa zaidi na kazi ya Alex Ferguson ambaye amestaafu kuinoa Man United.

Akaweka wazi kuwa bado hafurahii Man United inavyocheza na anaamini Moyes atakutana na mitihani kadhaa kabla ya kikosi chake kukaa sawa.

Zaidi angefurahia kuona Man United inashinda katika mechi ya wikiendi hii dhidi ya Manchester City.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic