Kocha Mkuu wa Man United, David Moyes
ametakiwa kumuonya kiungo wake, Ashley Young kuacha mara moja tabia ya
kujiangusha.
Young alijiangusha mara mbili leo katika
mechi dhidi ya Crystal Palace, mara moja mwamuzi akampa kadi ya njano na mara
ya pili akadanganyika na kutoa penalty.
Man United ilishinda mechi hiyo lakini
wachambuzi wa Sky Sports wameeleza tabia hiyo ya Young ni udangayifu katika
mchezo wa soka.
Mmoja wa wachambuzi hao, Tony Adams
aliyewahi kuwa nahodha wa Arsenal, alisema Young anaonyesha kiasi gani kwamba
analazimika kudanganya ili kuisaidia timu yake kushinda.
“Moyes amuonyesha, asipofanya hivyo
itaonekana kuwa anachofanya Young ni maagizo au mafunzo,” alisema Adams.
Young amekuwa akilalamikiwa kutokana na
tabia yake ya kuwadanganya waamuzi na kujiangusha ili kusababisha timu nyingine
iadhibiwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment