Mabingwa Yanga wamejiongezea pointi tatu
baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Bao pekee la Yanga lilipatikana katika
dakika ya 63 kupitia kwa Hamis Kiiza baada ya kuunganisha krosi safi ya Mrisho
Ngassa aliyemtoka Stephano Mwasyika na kupiga krosi safi.
Ngassa aliyekuwa anaicheza Yanga kwa
mara ya kwanza msimu huu, mwanzo alionekana tatizo kwa mabeki wa Shooting
lakini baadaye walifanikiwa ‘kumtuliza’.
Mechi hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa
huku Ruvu inayonolewa na Boniface Mkwasa ikicheza soka la kibabe la England
huku ikichanganya pasi kama La Liga.







0 COMMENTS:
Post a Comment