Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe amesema anataka kufunga mabao zaidi kila atakapopata nafasi, lakini ikitokea ikashindikana, zaidi anapenda kutoa pasi zinazozaa mabao.
Akizungumza jijini Dar, Tambwe raia wa Burundi
alisema hakunamchezaji anayeweza kufunga kila kukicha.
“Ili ufunge, wenzako watakupa pasi. Kama
imetokea uko katika nafasi hauwezi kufunga, vizuri ukatoa pasi.
“Sifa ya mshambuliaji mzuri ni yule
anayefunga lakini pili, yule anayetoa pasi zinazozaa mabao.
“Mnapocheza pamoja mnakuwa timu na
lengo ni kuisaidia timu, ndiyo maana unaona sipendi uchoyo, natoa kwa kila
aliyekuwa kwenye nafasi ya kufunga. Lakini nikiona naweza kufunga, nafanya
hivyo mara moja,” anasema Tambwe.
Tayari Tambwe ana mabao 6 na ndiye
anaongoza listi ya wafungaji bora wa Ligi Kuu Bara.
Kesho, Mrundi huyo anashuka dimbani na
kikosi cha Msimbazi kuwavaa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.







0 COMMENTS:
Post a Comment