Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba
dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, utatumika kwa ajili ya kuijaribu mitambo ya Azam TV,
imefahamika.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku
chache baada ya Kampuni ya Azam kupitia kituo chake cha Azam TV kuingia mkataba
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya mechi
za ligi hiyo.
Partick Kahemele ambaye ni mratibu wa
televisheni hiyo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, wataalam wao mpaka sasa
wanaridhishwa na maendeleo ya mchakato wa kukamilisha urushwaji wa matangazo
hayo, ambapo baada ya kuijaribu wiki iliyopita, sasa watatua Taifa kwa ajili ya
kazi hiyo.
“Tulishaijaribu kwa mara ya kwanza
wiki iliyopita wakati Azam FC ilipokuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
Ashanti kwenye Uwanja wa Chamazi. Wataalam wetu hawajaridhika, lengo lao kubwa
wanataka ubora wa kimataifa,” alisema Kahemele.
0 COMMENTS:
Post a Comment