Uongozi wa Yanga, umefanya kikao cha siri
katika kuamua wapi wataificha timu yao kabla ya kuumana na Simba, lakini wakapata jibu moja kwamba Kisiwani Pemba,
ndiyo sehemu muafaka.
Taarifa ilizozipata SALEHJEMBE, zimelifikia
inasema kuwa uongozi wa klabu hiyo uliyo chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji,
umekubaliana kwa pamoja kwamba wakakifiche kikosi chao hicho Pemba, sehemu
ambayo waliweka kambi msimu uliopita, kabla ya kucheza na Simba, katika mchezo
wa marudiano, ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Chanzo hicho, kutoka ndani ya Yanga,
kimeleeza kuwa kabla ya maamuzi hayo, awali Yanga walikubaliana kuwa kikosi
chao hicho kitaweka kambi jijini Mwanza, ambako wangecheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya APR ya Rwanda, ratiba ambayo ilivunjwa ghafla, huku sababu zikiwa siri
nzito na kuihamishia Pemba.
Chanzo hicho, kimeeleza kuwa mara baada ya
Yanga, kumaliza mchezo wao wa kesho dhidi ya Kagera Sugar, utakaopigwa katika
Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, kikosi hicho kitarejea jijini Dar, siku ya
Jumapili kwa ndege na kuondoka Jumatatu kwenda kisiwani humo.
“Tulishakubaliana kuwa timu itabaki Mwanza
kwa kambi, lakini tumekutana tena jana (juzi) katika kikao kingine na kuvunja
ratiba hiyo, siwezi kukwambia sababu hiyo ni siri yetu, lakini sasa tutaweka
kambi Pemba, tutarudi Dar siku chache kabla ya mechi,” kilisema chanzo na
kuongeza:
“Sasa hivi tunaelekeza nguvu zetu katika
mchezo dhidi ya Kagera, tunataka kuhakikisha tunashinda ili tukiingia katika
maandalizi ya Simba tuwe na morali ya hali ya juu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment