October 11, 2013




Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa katika timu ambazo anajitahidi kutokosa mechizao zao katika Ligi Lii Bara, msimu huu ni zile za Mbeya City kwa kuwa ameona timu hiyo inachangamsha ligi.


Kim amesema kuwa Mbeya City ni timu mpya katika ligi ila ndiyo inayofanya vizuri na kuonyesha changamoto kwa timu kongwe.

Alisema kuwa hawezi kusema ni wachezaji wangapi kutoka Mbeya City au kwingine ambao amewaona lakini bado anaendelea na kuangalia vipaji kwenye ligi nzima kwa jumla.

“Mpaka sasa kuna baadhi ya wachezaji ambao tayari ninao katika orodha yangu ila siwezi kusema kwani bado ligi inaendelea, hivyo na mimi naendeleo kutafuta wengine.

“Mbeya City ni kati ya timu ambazo nimeanza kufikiria wachezaji kutoka humo ndiyo maana siwezi kukosa mechi yoyote inayochezwa na timu hii hata ya ile waliocheza na JKT Oljoro nilienda Arusha,” alisema Kim.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic