Baba mzazi wa
mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, mzee Khalfan Ngassa amefurahi kuona
mwanaye huyo akifunga bao la kuokoa nyumba zake, lakini akamtumia ujumbe maalum
wa karipio, juu ya ahadi yake hiyo.
Khalfan amesema hakuweza kuushuhudia mchezo huo wa Simba na Yanga kutokana na kuwa na kazi ya kumalizia msiba wa mama yake mzazi, lakini hataki kusikia tena ahadi kama hizo zenye hatari, ambazo wakati mwingine ni vigumu kutekelezeka.
Mzee Khalfan ambaye ni
kiungo wa zamani wa Pamba na Simba, amesema awali alivyosikia ahadi hiyo ya
Ngassa kupitia gazeti hili, alishtuka vibaya, ambapo alilazimika kumtafuta
Ngassa lakini hakuweza kumpata na kumtaka kuhakikisha anakuwa makini katika
kuangalia mambo ya kuahidi.
“Nilishtuka sana baada ya
kuona taarifa zile, lakini sikuwa mimi peke yangu, hata dada zake walishtushwa
na taarifa ile, nikawaambia wawe na subira nimtafute kwanza Ngassa, ili
nimuulize lakini sikumpata,” alisema mzazi huyo na kuongeza:
“Nashukuru ameweza
kuondoa sintofahamu hiyo kwa kufunga, ni jambo zuri lakini sitaki kusikia tena
juu ya ahadi kama hizo, ni hatari sana, inawezekana alidhani amezungumza jambo
dogo lakini kwa mechi ya Simba na Yanga, ile ni hatari kubwa.”
Kauli hiyo inakuja
kufuatia siku chache kabla ya mechi ya Simba na Yanga, mshambuliaji huyo kuahidi
endapo atashindwa kufunga au kutoa pasi ya bao, angeweza kuchoma moto nyumba
zake tano, ingawa alifanikiwa kufunga bao la kwanza kwenye mechi hiyo
iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment