Mshambuliaji wa zamani wa Yanga raia wa Kenya, Ben Mwalala,
amesema kuwa ili Yanga iweze kuwa na wachezaji wazuri baadaye, inabidi ielekeze
macho yake kuwanoa vijana wenye umri wa chini ya miaka ishirini (U-20) kuliko
kununua wachezaji wa kigeni kwa gharama kubwa.
Mwalala amesema kuwa kwa muda mrefu timu hiyo imekuwa na kawaida ya
kununua wachezaji wa kigeni kwa gharama kubwa wakati wengine viwango vyao ni
vidogo.
“Ili Yanga baadaye iweze
kuwa na hazina ya wachezaji wazuri kama timu ya Simba, inabidi iwekeze kwa
vijana wa chini ya umri wa miaka ishirini,” alisema.
Aidha, kwa upande
mwingine aliwashauri viongozi wa timu za hapa nchini kuacha kuingiza siasa
katika masuala ya soka.
“Unakuta kiongozi wa
ngazi ya juu ya klabu anaingilia kazi za kocha na kuingiza mambo ya siasa
katika timu, hali ambayo husababisha migogoro na kushusha kiwango cha soka cha
timu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment