Mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, amepiga
mabao manne katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderlecht ya
Ubeligiji ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Katika mabao hayo, moja lilikuwa bonge
la bao ambalo alipiga shuti kali lenye kasi ya maili 93 kwa saa na baada ya
mechi, mara moja akakabidhiwa mpira.
Miezi michache iliyopita, mshambuliaji
Amissi Tambwe wa Simba, alifunga mabao manne katika mechi dhidi ya Mgambo
Shooting, lakini mwamuzi akamyima mpira.
Hali hiyo ilisababisha kuzuka kwa
mjadala mkubwa na mwamuzi akasisitiza alipewa maagizo ya kutompa mpira huo
kutokana na gharama kubwa.
Lakini mambo ya Ulaya tofauti, angalia
katika picha Ibra Cadabra akiwa na mpira wake mara tu baada ya kufunga bao zake
nne. Kawaida mchezaji hupewa mpira kila anapofunga bao tatu au hat trick.
0 COMMENTS:
Post a Comment