Mabao mawili yaliyofungwa na mabeki
wa Simba, yameleta tatizo katika cha timu hiyo, ambapo sasa ni wazi safu hiyo
itafumuliwa na kusukwa upya.
Uchunguzi uliofanywa na blogu hii, umebaini kuwa benchi la ufundi la
kikosi hicho, limegundua udhaifu mkubwa katika majukumu ya ukabaji, ambayo
yalizalisha mabao mawili ya vichwa, kutoka kwa mabeki wa Simba Joseph Owino na
Gilbert Kaze na tayari mikakati ya kuyamaliza imeanza.
Katika mazoezi ya jana asubuhi ya
kikosi hicho, kocha wa timu hiyo, Ernie Brandts, na wasaidizi wake Fred Felix
Minziro na Razak Siwa walionekana kuwapa mazoezi nyota hao, katika mipira ya
kona, ambapo jumla ya kona 10 zilitosha kuonyesha tatizo.
Wakati wa zoezi hilo, makocha walipata
nafasi ya kuyaona mabao kama yale yaliyofungwa Jumapili iliyopita, ambapo
washambuliaji Shaban Kondo na Hussein Javu, walifunga kila mmoja bao moja ndani
ya kona kumi zilizopigwa.
Wakati mabao hayo yakifungwa,
wafungaji wote walifunga kirahisi bila kukabwa, ambapo tayari makocha hao
wametoa maelekezo maalum juu ya tatizo hilo.
Hata hivyo, SALEHJEMBE limebaini kuwa,
safu hiyo ya ulinzi, inaweza kuwa na mabadiliko makubwa katika mchezo wa leo
dhidi ya Rhino Rangers, ambapo sura mpya akiwemo kipa Deogratius Munishi ‘Dida’
anaweza kuanza.
Mbali na Dida, nahodha wa timu hiyo,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, anaweza kupumzishwa katika mechi hiyo, ingawa kocha
wake Brandts, ameonekana kutotaka kuweka wazi juu ya nyota watakaoweza
kupumzishwa katika mechi ya leo, akisema hilo litajulikana katika kikao cha leo
mchana.
0 COMMENTS:
Post a Comment