Cristiano Ronaldo ametofautiana moja kwa moja na kocha wake wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho.
Ronaldo ametofautiana na kauli ya mwanzo ya kocha huyo aliposema Hispania watu wengi ni wabaguzi wakubwa.
Lakini Rolando ameeleza kwamba anafurahishwa na maisha ya Hispania na asingependa kuingia alipofikia Mourinho.
“Sitaki kuingia huko, najua hili linanigusa kwa kuwa pia ni Mreno, lakini hapa ni sehemu ninayoipenda na ninafurahia maisha ya Hispania.
“Ningependa kusema hapa ni sehemu ambayo najisikia niko nyumbani na watu wa Madrid siku zote wameonyesha upendo wa hali ya juu kwangu,” alisema Ronaldo.
Pamoja na Ronaldo kusema maneno hayo, kiutamaduni inaelezwa Wahispania wamekuwa wakiwadharau Wareno na kuwaona watu wa hali ya chini.
Hali hiyo imemfanya Mourinho kuingia katika vita na Wahispania ingawa imekuwa ya kimyakimya na ndiyo sababu kubwa kwake kuamua kuondoka Madrid na kurejea Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment