October 23, 2013



Mgombea wa Urais, katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,leo amezindua kampeni zake katika nafasi hiyo.


Uzinduzi huo, uliofanyika katika hoteli ya Hyat Regency, jijini Dar, Malinzi ametumia takribani saa moja na nusu, kueleza nia ya kutaka nafasi hiyo kikubwa akilenga mabadiliko ndani ya TFF.


Malinzi, amesema endapo atapata ridhaa ya kuongoza TFF, moja ya mabadiliko makubwa yatakuwa katika kitengo cha ufundi cha shirikisho hilo ambapo atahakikisha mabadiliko makubwa yanafanyika likiwamo suala ka kuongeza bajeti ya kifedha.


Malinzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Kagera amesema mbali na suala hilo pia atahakikisha soka la vijana linapewa kipaembele kwa kuweka mipangio itakayotekelezeka kirahisi huku akitaka apewe siku 100 ili kuweza kupima mabadiliko atakayoyafanya

Pamoja na hivyo, Malinzi alizungumzia mambo mbalimbali kama vile suala la kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana, mafunzo ya waamuzi na pia kuzijali timu za taifa.

Alisisitiza nataka kuona mpira unachezwa nchi nzima huku akitolea mfano namna ambavyo watu huchezesha mpira wakiwa wamevaa suruali za kawaida.

Malinzi alizungumzia suala la kukosekana kwa magari ya kubebea wagonjwa kwenye mechi mbali za soka na mambo mengine mengi ambayo tutaendelea kukuletea taratibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic