Dar es Salaam: Bia ya Kilimanjaro Premium Lager
imeleta msisimko mpya katika utani wa jadi kati ya
mashabiki wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia
kampeni yake mpya ijulikanayo kama NANI MTANI
JEMBE iliyozinduliwa leo jijini Dar es salaam na itadumu
kwa muda wa miezi miwili.
Akiongea kwenye uzinduzi, George Kavishe, Meneja wa
bia ya Kilimanjaro Premium Lager amesema NANI MTANI JEMBE itawapa fursa ya aina yake
mashabiki wa Simba na Yanga kuonyesha mapenzi yao kwa Simba na Yanga kupitia kampeni hiyo
itakayoendeshwa kwa sms ambapo Shilingi milioni 100 zitagawanywa kati ya Simba na Yanga halafu fedha
hizo zitawekwa katika benki maalum mtandaoni.
¸ Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE
itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha
shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa.
¸ Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi
cha shilingi milioni 50.
¸ Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani
Jembe akibandua ganda la kizibo cha Bia ya Kilimanjaro.
¸ Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga
kura zaidi na kuichangia zaidi.
¸ Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida
cha kutuma sms na baada ya mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa
uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya
kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha
hizo katika miradi yake ya maendeleo.
Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani
kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao.
Mbali na kampeni ya SMS, kutakuwepo na shilingi milioni 2 ambazo mashabiki watajishindia
kila wiki kwa wiki kumi kwa mashabiki watakaoshiriki zaidi. Vilevile Nani Mtani Jembe
itawaburudisha mashabiki wa Simba na Yanga kupitia matukio mbalimbali mabonanza, promosheni
zitakazofanyika barabarani, kwenye bar na kwenye matawi ya Simba na Yanga.
Kampeni hii itafika
kileleni tarehe 14 Disemba 2013 ambapo mechi ya hisani itachezwa kati ya klabu hizo mbili kwenye
Uwanja wa Taifa mbele ya maelfu ya mashabiki wa timu hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment