October 6, 2013




Mabingwa Yanga, wameichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Mabao ya Yanga yalifungwa na Mrisho Ngassa halafu akatoa pasi kwa Didier Kavumbagu ambaye alipachika bao la pili.

Mechi ilikuwa na ushindani mkubwa katika Yanga walionekana kuwa fiti na kujiandaa vilivyo kushinda katika mechi hiyo.

Ngassa alionyesha uwezo mkubwa na kuwa tatizo kubwa kwa mabeki wa Mtibwa Sugar waliokuwa wakijaribu kumzuia.

Kutokana na ushindi ushindi, Yanga wamefikisha pointi 12 na kuchuka kutoka nafasi ya nane hadi ya tatu nyuma Azam FC na vinara Simba.



Matokeo mengine ya ligi kuu leo, Prisons ikiwa ugenini mjini tanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 baada ya kuwachapa Mgambo.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakika ya 62 na Peter Michael.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic