Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross)
limesema watu 21 walianguka na kupoteza fahamu wakati wa mechi ya watani Simba
na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Watu walikuwa wakianguka mfululizo kila
Yanga ilipofunga bao, likianza bao la Mrisho Ngassa. Baadaye mawili
yaliyofungwa na Hamis Kiiza.
MAMA YANGA |
Watu wa Red Cross walionekana
kuchanganyikiwa kutokana na watu kuanguka mfululizo, wakati mwingine
wakalazimika kuwabeba kwa mikono kutokana na vifaa kuwa vichache.
Mmoja ya walioanguka na kuzimia ni
shabiki maarufu wa Yanga anayejulikana kama Mama Yanga.
Angukaanguka hiyo ilianza kuonekana
upande wa Simba na hasa kipindi cha pili, mara tu baada ya timu hiyo kuanza
kusawazisha.
Timu hizo zilimaliza mechi hiyo kwa sare
ya mabao 3-3 wakati Yanga ikifunga mabao yake katika kipindi cha kwanza na
Simba ikasawazisha yote katika kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment