BARTHEZ AKIDAKA MPIRA MBELE YA MWOMBEKI WA SIMBA, LEO. |
Sare ya 3-3 ya Simba na Yanga leo,
inaonekana haiwezi kwenda hivihivi bila ya mchawi kusakwa.
Tayari Simba wamesema kuna watu
wanawahujumu, Yanga pia wametamka waziwazi kwamba wana hofu na kipa wao, Ally
Mustapha ‘Barthez’.
HUMUD (KUSHOTO) NA CHANONGO (KATIKATI) WAKIWANIA MPIRA |
Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni
amesema wazi amekerwa na baadhi ya wachezaji wanaofanya makusudi kuwahujumu.
“Wanataka kutuhumu kwa makusudi,
hawataki kucheza mpira na wanafanya makusudi kutuangusha.
“Tulipoingia vyumbani wakati wa
mapumziko, nikawaambia kama kutuhujumu na kuiachia Yanga mabao matatu, basi
inatosha, basi kipindi cha pili tucheza mpira.
“Utaona vijana walioingia wamefanya
vizuri na wamecheza na kuleta mabadiliko, lakini ikifika wakati nitawaja hawa
wanaofanya huu upuuzi,” alisema Kibadeni.
Katika mchezo huo aliwatoa Haruna
Chanongo na Abdulhalim Humud na kuwaingiza Luciano na Sain Ndemla ambao ni
makinda lakini wakabadili mchezo.
Kwa upande wa Yanga, mmoja wa viongozi
wa vijana, Bakili Makele alisema wana hofu kutokana na mabao aliyofungwa
Barthez.
“Kweli umefika wakati wa uongozi
kuchukua hatua, hii si haki. Mabao aliyofungwa Barthez si sahihi na yanaonyesha
kuna chembe za hujuma.
“Si leo tu, hata Kagera na kwingine haya
mambo yalitokea. Imenikera na tumeumia sana kama Wanayanga,” alisema akionyesha
jazba.
Hata hivyo, mabao waliyofungwa Yanga
yanaonyesha wazi yalikuwa makosa ya mabeki na wala si kipa huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment