Mwenyekiti
wa Mtibwa Sugar, Hamad Yahya ameweka historia kwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa
Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board).
Katika
uchaguzi uliofayika leo, Yahya ameshinda kwa ulaini kwa kuwa alikuwa mgombea
pekee katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano katika jengo la
Golden Jubilee Tower katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Yahya
alipata kura zote kumi za ndiyo, huku klabu tatu za jeshi zaJKT Ruvu, Mgambo
Shooting na na Rhino Rangers pamoja na Coastal Union, zikishindwa kuhudhuria.
Mwenyekiti wa Azam FC, Said Muhammad Said Abeid pia ameweka rekodi ya kuchukua cheo hicho kwa kuchaguliwa kwa mara ya kwanza. Pia hakuwa na mpinzani.
Wajumbe
wawili wa Kamati ya Uendeshaji,Khatibu Mwindadi wa Mwadui na Kazimoto Miraji
Muzo wa Pamba, wameibuka washindi katika kura za klabu za Ligi Daraja la Kwanza
(FDL).
Muzo alipata kura 15 za ndiyo wakati mbili zikimkataa, huku Mwindadi akipata kura 16 na moja ilimkataa. Klabu za FDL ambazo hazikuhudhuria uchaguzi huo ni Transit Camp, Burkina Faso, Polisi Mara, Stand United, Toto Africans, Polisi Tabora na Kanembwa JKT.
0 COMMENTS:
Post a Comment