Raphael Varane amerejea katika kikosi cha Real Madrid baada ya kushindwa kuichezea timu yake ya taifa ya Ufaransa.
Mara tu baada ya kurejea amerudishwa kwenye uangalizi wa kitengo cha afya cha Real Madrid ili kuangalia vizuri afya yake.
Hali hiyo inatokana na afya ya goti lake ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda sasa na kusababisha akae benchi.
Bwana mdogo huyo tayari alishampora namba Pepe ambaye sasa amerejea tena katika kikosi cha Real Madrid.
Varane aliikosamechi dhidi ya Finland baada ya kukosa mazoezi ya timu ya taifa ingawa alikuwa kati ya wachezaji walioitwa na kocha Didier Deschamp.
0 COMMENTS:
Post a Comment