Waamuzi hawa watatu, Sánchez Arminio, López Nieto na Puentes Leira, lazima mmoja wao atapewa kazi ya kuichezesha mechi ya watani wa jadi Real Madrid dhidi ya Barcelona.
Imeelezwa Jumanne ijayo ndiyo atatangazwa mwamuzi mmoja ambaye atakuwa kati kucheza mechi hiyo maarufu kama El Clasico inayosubiriwa kwa hamu.
Mechi hiyo imepangwa kupigwa Oktoba 26 na inaonekana tayari imekuwa gumzo kubwa katika soka duniani.
Imeelezwa sababu kuu nne zinazofanya waamuzi hao watatu wawe na vigezo vya kuichezesha El Clasico ni hizi.
1)Lazima awe mwamuzi wa kimataifa kutoka Hispania ambaye anatambulika kimataifa na hasa na mashirikisho mawili ya Fifa na Uefa.
2) Asiwe anatokea Madrid au Catalonia. Hali hiyo imesababisha wabaki watatu, wengine mahiri na maarufu kama Estrada Fernández, Del Cerro Grande na Velasco Carballo, wamekosa nafasi hiyo/
3) Pia hatakiwi kuwa amechezesha mechi ya Barça nyumbani au Madrid ugenini katika msimu huu na hicho ndiyo kimewang’oa (Teixeira na Muñiz), hii ni sheria kabisa.
4) Pia sheria inasisitiza, ndani ya miezi michache, mwamuzi hatakiwi kuwa ameshiriki katika mechi yoyote ya timu hizo na hii inamuondoa mwamuzi mahiri Mateu.
Lakini kitu kizuri, mwamuzi atakayepewa nafasi ya kuchezesha, ndiye anakuwa na uwezo wa kuchangua mwamuzi wa akiba katika mechi atakayoiongoza.
0 COMMENTS:
Post a Comment