Wazungu wameendeleza unafiki wao kuhusiana na suala la ubaguzi wa
rangi baada ya mashabiki wa CSKA Moscow kumbagua waziwazi kiungo Yaya Toure wa Manchester
City.
Mashabiki hao wenye roho mbaya ambao wamekuwa wakidanganya kwamba
wana mapenzi na Waafrika walionyesha vitendo vya nyani ikiwa ni ishara ya
ubaguzi wa rangi kwa Toure raia wa Ivory Coast.
Manchester City ilikuwa nyuma kwa bao moja, Toure akaonekana kuwa
tatizo kutokana na kutoa pasi za uhakika ikiwemo ya bao la alilofunga Sergio
Ramos ambaye alifunga mawili.
Kuhusiana na hilo, kupitia mtandao wa Twitter, Toure alisema: “Inakatisha
tamaa kiasi fulani kwa watu kuendelea na vitendo hivyo.
TOURE NA AGUERO WAKIMUONYESHA MWAMUZI MASHABIKI WALIOKUWA WAKIONYESHA ISHARA YA NYANI KUMBAGUA TOURE. |
“Najisikia vibaya, lakini bado siwezi kukata tamaa kwa kuwa wengi
wananipenda na kuniunga mkono.”
0 COMMENTS:
Post a Comment