October 23, 2013


Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya zimemalizika huku wachezaji nyota duniani wakionyesha uwezo wao katika upachikaji mabao.
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amefunga mabao manne pekee wakati PSG ikiichapa Anderlecht mabao 5-0 ikiwa nyumbani kwa Ubelgiji.


Zlatan amefunga mabao hayo manne huku mshambuliaji mwingine nyota wa PSG, Edinson Cavani akipiga bao moja.


Cristiano Ronaldo naye ameisaidia Real Madrid kupata ushindi baada ya kufunga mabao mawili yaliyoiua Juventus ya Italia kwa 2-1.


Mechi hiyo ilikuwa ya kuvutia zaidi katika zilizochezwa jana na pamoja na kuwa ugenini, Juventus walionyesha kiwango cha juu kabisa.


Mabingwa watetezi Bayern Munich nao wakaonyesha cheche kwa kuwachapa Shakhtar Donestik kwa mabao 4-0, huku mchezaji bora Ulaya, Frank Ribery akipiga mbili.

Didier Drogba akaiongoza Galatasaray ikiwa nyumbani kwa kuwachapa Copenhagen kwa mabao 3-1. Drogba akitupia moja, Melo na Sjneider.

Manchester United ikaenda kileleni mwa Kundi A baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad, shukurani kwa bao la kujifunga la Inigo Martnez.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZILIZOCHEZWA
Bayern Munich 4-0 Viktoria Plzen
Man United 1-0 Sociedad
Galatasaray 3-1 Copenhagen
Real Madrid 2-1 Juventus
Anderlecht 0-5 PSG
Benfica 1-1 Olympiakos
Beyer Leverkusen 4-0 Shakhtar


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic