Baraza la Wazee wa Yanga, wamekubali
maamuzi ya uongozi wa timu hiyo kuwa kampuni itakayoendesha na kusimamia mali
zao.
Kauli hiyo, wameitoa ikiwa ni siku moja
uongozi huo kutoa mapendekezo ya maoni kwa wanachama wake wote nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akirimali alisema maamuzi hayo wameyatoa baada
ya kuwepo ya wazee wote.
Akilimari alisema, kwa mujibu wa
makubaliano hayo wamefikia maamuzi ya timu kuingia asilimia 51 ya hisa, hivyo
wametaka wanachama kutoa maoni ya ndiyo ili kuiboresha klabu yao.
“Baraza la wazee wa Yanga kwa pamoja
tumekubaliana timu yetu kuwa Yanga kampuni na siyo Yanga asili.
“Lengo letu likiwa mali zetu zote
zisimamiwa, hivyo tunawataka wanachama wote nchini nao kutoa maoni ya ndiyo
kwenye sanduku la maoni lililopo klabuni,” alisema Akirimali.
mwisho
0 COMMENTS:
Post a Comment