October 17, 2013





Kiungo wa Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto amesema ataendelea kupambana pamoja na ugumu wa ligi hiyo.

Mtanzania huyo ameonyesha uwezo na kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Al Markhiya inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Qatar.


 “Ligi kweli ni ngumu sana, unajua ushindani unatokana na timu za hapa kuwa na uwezo wa kifedha.

“Maana yake wachezaji kutoka Ulaya, Amerika Kusini na hasa Brazil na Argentina wamejazana hapa.

“Hivyo kila mmoja anajituma na mimi nimekuwa nikipambana kuhakikisha natoa msaada katika timu yangu,” alisema Kazimoto ambaye sasa ndiye tegemeo namba nane katika kikosi cha timu hiyo.
Kwa mfumo wa Qatar, baadhi ya wachezaji wa ligi kuu wamekuwa wakiruhusiwa kucheza katika mechi za daraja la kwanza hasa kama wanakuwa hawazichezea timu zao za ligi kuu katika timu husika.

Vikosi vya pili vya timu zinazoshiriki ligi kuu, viko katika ligi daraja la pili, hivyo nyota kadhaa wa ligi kuu wamekuwa wakishuka kwenda kuchezea timu hizo na kuongeza ushindani zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic