Mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa,
Ismail Aden Rage amerejea nchini na kuahidi kumwaga ugali kwa kuwa
waliomsimamisha wamemwaga mboga.
Rage amerejea nchini Saa 1 na ushee
usiku akitokea nchini Sudan na kusisitiza kwamba atazungumza kesho saa saba
mchana kwenye makao makuu ya klabu hiyo.
MASHABIKI WACHACHE WALIOJITOKEZA KUMPOKEA |
Rage alipokelewa na mashabiki wapatao
120 waliokuwa katika mabasi matatu ya kukodi, ambao walikuwa wakiimba nyimbo za
kuonyesha wamekwenda kumpokea.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI |
Hata hivyo ilionekana wazi mashabiki hao
wengi hawakuwa wanachama wa Simba, na idadi yao haikuwa kubwa kama ambavyo
ilitarajiwa awali.
Baada ya kutoka alizungumza na waandishi
wa habari halafu akaingia kwenye gari aina ya Toyota na kuondoka zake hadi
klabu ambako alitoa ahadi hiyo ya kumwaga ugali kesho.
Rage alisimamishwa kwa madai ya
kutoshirikiana na viongozi wenzake ikiwemo kamati ya utendaji na maamuzi ya
mambo mengi alikuwa akifanya mwenyewe.
Pamoja na hivyo suala la kumuuza
mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa Etoile du Sahel ya Tunisia, hadi leo Simba
inadai dola 300,000 na haijalipwa kitu.
Lakini aliingia mkataba na Azam TV ili
Simba TV iwe inaonyeshwa na kulipwa Sh milioni 330 kwa miaka mitatu ikiwa na
maana kila mwaka Simba itapata Sh milioni 110, wakati kampuni ya Zuku ilikuwa
tayari kutoa dola 300,000 kwa mwaka na walikuwa bado kwenye mazungumzo.
PICHA: LENZI YA MICHEZO
0 COMMENTS:
Post a Comment