December 23, 2013


MUSOTI AKIWA NA KATIBU MKUU WA SIMBA, EVODIUS MTAWALA (KATIKATI) NA KAIMU MWENYEKITI WA SIMBA, MZEE KINESI

Beki ngangari wa Simba, Donald Musoti, amekiangalia kikosi cha Yanga, baadaye akaibuka na hoja nzito kuwa washambuliaji wa timu hiyo hawana madhara makubwa lakini pia akagusia kuhusu beki, akaongeza kuwa ni nyanya kabisa.


Musoti, raia wa Kenya, amesema awali alikuwa na wasiwasi juu ya sifa walizokuwa wakipewa washambuliaji wa Yanga lakini amegundua kuwa si lolote.

Musoti, ambaye amehamia Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya, amesema wakati hali ikiwa hivyo kwa washambuliaji, pia amegundua kuwa, safu ya ulinzi ya Yanga ni nyepesi zaidi ambapo mabeki wao ni laini.

“Unajua wakati nafika, nilikuwa nasikia kelele nyingi kuhusu washambuliaji wa Yanga kuwa ni wazuri sana, kiasi fulani nilianza kupata woga, lakini nimegundua kuwa ni kelele tu, hawana lolote la kutisha.


“Ukiacha washambuliaji, angalia pia hata hao mabeki wao ni wepesi sana, sijaelewa ni kwa nini, lakini nimegundua kuwa ni laini sana, beki huwezi kuwa mwepesi kupitika kiasi kile, nasikia kuwa wanashiriki Klabu Bingwa Afrika, wana kazi kubwa ya kufanya kama wanataka kupata mafanikio,” alisema Musoti.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic