December 11, 2013



Kipa Ivo Mapunda ameamua kurejea nchini baada ya kukubali kuingia mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba.
Mapunda aliyekuwa anakipiga Gor Mahia ya Kenya, ametua Simba ramsi na atasaini mkataba wa kuichezea timu hiyo mara moja.


“Kweli nimekubaliana na Simba, kila kitu kimekwenda vizuri lakini sasa nataka kuelekeza nguvu zangu katika michuano ya Chalenji kwanza,” alisema Ivo.
IVO AKIWA MAZOEZINI KWENYE UWANJA WA CITY JIJINI NAIROBI WAKATI AKIICHEZEA GOR MAHIA

SALEHJEMBE ilikuwa ya kwanza kuhusiana na mafanikio makubwa aliyoyapata Ivo akiwa Kenya na timu ya Gor Mahia ambayo aliisaidia kupata ubingwa wa Ligi Kuu Kenya.

Mapunda sasa ni kipa namba moja wa Kili Stars inayoshiriki michuano ya Chalenji na kesho itacheza na Zambia kusaka mshindi wa tatu baada ya kufungwa na Kenya kwa bao 1-0.
IVO AKIWA NA SALEH ALLY WALIPOKUTANA JIJINI NAIROBI NA KUFANYA MAHOJIANO KUHUSIANA NA MAISHA YAKE NCHINI KENYA, PIA TAULO LAKE LILILOPATA UMAARUFU MKUBWA.

Ivo anarejea kufanya kazi chini ya Logarusic ambaye walikuwa pamoja Gor Mahia msimu uliopita kabla ya kocha huyo kwenda kwao Croatia na kugoma kurejea Nairobi.

Tayari Simba imemsajili Yaw Berko raia wa Ghana kuichezea kwa miezi sita tu.

Maana yake, kipa kinda wa Simba, Abuu atakuwa hana nafasi tena ya kucheza katika kikosi cha kwanza kama ambavyo alifanikiwa katika mzunguko wa kwanza.

Tayari Simba imeishaamua kuachana na kipa Abel Dhaira ambaye imeeleza kuwa kiwango chake kimeporomoka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic