| NIKIWA NA MZEE SMALL MAENEO YA TABATA, KARIBU KABISA NA NYUMBANI KWAKE. HII ILIKUWA LEO MCHANA. |
Said Ngamba maarufu kama Mzee Small
amesema kweli anaumwa lakini amekuwa akiendelea kujiuguza.
Mzee Small alizushiwa kifo kupitia
mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook jana usiku, amesema alizipokea
taarifa hizo kwa mshangao.
“Kweli inashangaza, vipi watu waamue tu
kukuzushia eti umekufa, wameuliza wapi na nani kawaeleza, kitu cha ajabu sana.
“Lakini nipo na Mungu ndiye anapanga,
siku ya mwisho atatoa jibu kuhusiana nami kwamba mwisho umefika au la,”
alisema.
SALEHJEMBE ilimtembelea Mzee Small hadi
nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam na kusema amekuwa akiendelea na
mazoezi.
| NIKIWA NA MZEE SMALL NA MKEWE MAMA SAID TUKIELEKEA NYUMBANI KWAO AMBAKO NILIKUNYWA SOKA KAMA MGENI...HEHE |
“Nafanya mazoezi kwa ajili ya
kujiimarisha zaidi kiafya, ni kazi ngumu lakini najitahidi kwa kuwa upande
mmoja wa mwili wangu hauna nguvu, naweza kusema umepooza,ndiyo maana wakati mwingine nalazimika kutumia fimbo ili kutembea vizuri,” alisema.
Taarifa za Mzee Small kwamba amefariki
dunia ziliwachanganya wengi hadi SALEHJEMBE ilipoandika na kueleza haikuwa
kweli.
Mkewe Mzee Small naye pia alisema
walishitushwa na taarifa hizo ambazo hawakuwa wamejua zimetokea wapi.







0 COMMENTS:
Post a Comment