Wakati Adel
Amrouche akitangazwa kuwa kocha bora wa michuano ya Chalenji iliyomalizika hivi
karibuni nchini Kenya, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema timu
yake ilionekana ni wasindikizaji.
Musonye
alisema kamati ya ufundi ya Cecafa imemteua Amrouche kuwa kocha bora wa
michuano ya Chalenji kutokana na kuwa na timu ambayo iliaminika haiwezi hata
kufika fainali.
“Lakini
imefika fainali na hatimaye imetwaa kombe,” alisema Musonye.
![]() |
| WACHEZAJI WA HARAMBEE STARS WAKIMBEBA JUUJUU BAADA YA KUTWAA KOMBE |
Kabla ya
hapo, Amrouche raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria alikuwa kocha wa timu
ya taifa ya Burundi na ilikuwa ikifanya vema pamoja na kuandamwa na ukata.
Lakini amekuwa
akionyesha uwezo mkubwa, sawa na alivyosema Musonye kwamba timu yake ilionekana
haina lolote.
![]() |
| AKIKABIDHIWA TUZO YA KOCHA BORA |
Lakini uchezaji
wa Harambee Stars katika michuano hiyo pamoja na kwamba haikuwa na wachezaji
wenye majina makubwa sana ulikuwa ni wa kiwango cha juu.
Mfano mzuri
ilipokutana na Tanzania Bara katika nusu fainali, Kenya ilitawala sana na hasa
kipindi cha kwanza.
Lakini Amrouche
anayesifiwa kwa uwezo mkubwa wa mipango, aliweka mbinu bora za kuwabana Mrisho Ngassa
na Mbwana Samatta na kweli akafanikiwa kuilaza Kili Stars bao 1-0 akasonga
fainali.
Bado wengi
hawakuipa nafasi timu hiyo, lakini ikaifunga Sudan mabao 2-0 na kufanikiwa
kutwaa kombe hilo lililokosekana Kenya kwa zaidi ya miaka saba.











0 COMMENTS:
Post a Comment