Siku chache baada ya kuachana na Ashanti
United, kipa mzoefu Amani Simba ameibuka na kutangaza kuachana na soka rasmi.
Wiki iliyopita Ashanti iliachana na
wachezaji wake watano kuelekea kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara,
akiwemo kipa huyo.
Ofisa habari wa timu hiyo, Marijani
Rajabu, amesema kipa huyo aliuandikia uongozi wa timu hiyo
barua ya kuacha kazi siku chache mara baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika
ambapo uongozi ulipitisha ombi hilo.
Amani
aliyeanza kucheza soka la ushindani tangu mwaka 1998, amesema kuwa ameamua
kufanya hivyo kwa kuwa anahitaji kupumzika na kuwaachia vijana waonekane na
kukuza vipaji vyao kwenye soka.
“Dah, nimecheza sana tangu mwaka 1998,
nafikiri muda wangu wa kupumzika na kuwaachia wengine umefika, wapo vijana
wengi wanahitaji kuonekana kwa hiyo inabidi tuwapishe nao pia waonyeshe uwezo
wao,” alisema Amani na kuongeza:
“Mimi tena sasa hivi soka langu na timu
zangu zitakuwa za maveterani, niliandika barua ya kuacha kazi Ashanti ni kwa sababu
hii na wala si nyingine kama watu wanavyodhani.”
Amani ameshachezea jumla ya timu tisa
katika ligi kuu mpaka sasa ambazo ni Tanzania Prisons, Moro United, Polisi
Moro, Mtibwa Sugar, Simba SC, Kagera Sugar, JKT Ruvu, Mbeya City na Ashanti
United.








0 COMMENTS:
Post a Comment