Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic leo
aliibuka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuufuatilia kwa karibu
mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Ashanti.
Katika mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda kwa
mabao 2-1, Logarusic alikuwa akishuhudia kwa umakini mkubwa.
Aliendelea kushuhudia akiwa karibu na bosi wa
kamati ya Ufundi ya Simba, Ibrahim Masoud ambaye pia alikuwa makini sana.
Baada ya mechi, Logarusic alipoulizwa,
alijibu kwa kifupi tu: “Nilikuja kuangalia mechi kama mashabiki wengine.
Simba inashuka dimbani kesho Jumapili kuuanza
mzunguko wa pili kwa kuwavaa Rhino ya Tabora.
0 COMMENTS:
Post a Comment