Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusi
amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi ya leo.
Simba inashuka dimbani leo kucheza mechi
yake ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza leo asubuhi amesema
wanaichukulia mechi hiyo kwa uzito mkubwa na pointi tatu ndiyo zitawapa dira
nzuri.
“Tukishinda leo ndiyo mwanzo unaweza
kutueleza tunaelekea wapi, kama tutapoteza, basi ni tatizo kubwa kwetu.
“Tumejiandaa na tuko safi tayari kwa
mchezo ingawa dakika 90 ndiyo zitatoa jibu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment