Wagosi wa Kaya jana walipoteza mchezo
wao wa kirafiki dhidi ya Fanja ya Oman inayovaa jezi za njano na nyeusi.
Pamoja na kupoteza mchezo huo wa jana,
chini ya Kocha Yusuf Chippo, Coastal imeendelea na mazoezi leo.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye uwanja
wa mazoezi unaomilikiwa na Shirikisho la Soka la Oman (Ofa) ulio katika eneo la
See jijini Muscat Oman.
Coastal ilifanya mazoezi yake na
itaendelea na ratiba huku ikitarajia kucheza mechi nyingine za kirafiki.
Wagosi wa Kaya watakuwa jijini Muscat kwa
wiki mbili katika kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
PICHA: COASTAL UNION SPORTS CLUB







0 COMMENTS:
Post a Comment