Shrikisho la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka
Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania
na Komorozine Sports ya Comoro.
Iwapo Yanga itaishinda timu hiyo ya Comoro katika mechi ya kwanza, maana yake itakuwa imejiweka katika mazingira mazuri ya kushinda mechi ya marudiano.
Kama Itashinda, basi Yanga itakuwa imevuka na hatua itakayofuata itakuwa ngumu zaidi kwake, kwani itakutana na Mabingwa Watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi
wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa
mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya
Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien
(Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya
Tanzania na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati
ya Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi,
Waleed Ahmed Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa
mechi hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya
michuano hiyo ni Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla
(Misri), Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly
Shandy (Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) limeteua waamuzi kutoka
Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania
na Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar
es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa
kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi
wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa
mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya
Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien
(Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya
Tanzania na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati
ya Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi,
Waleed Ahmed Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa
mechi hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya
michuano hiyo ni Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla
(Misri), Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly
Shandy (Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).

0 COMMENTS:
Post a Comment