| YUSUF ABEID AKIWAFUA MAKIPA HAO, LEO JIJINI MUSCAT |
Kipa nyota wa zamani wa Pamba ya Mwanza, Yusuf
Abeid ameendelea kuwanoa na kuwapa ‘maujuzi’ makipa wa Coastal Union, Shaaban
Kado na Said Lubawa.
Abeid ni raia wa Oman mwenye asili ya Tanzania, aliendelea
na mazoezi katika uwanja unaomilikiwa na Shirikisho la Soka la Oman (Ofa)
kwenye eneo la Seeb. Abeid ni mzaliwa wa Kigoma aliyefanya vizuri sana akiwa na
Pamba ya Mwanza.
Abeid pia ni kati ya wakufunzi wa makipa wa makocha wa makipa wa Ofa na anatambuliwa pia na Shirikisho la Soka la Asia (AFC) na lile la Kimataifa (Fifa).
Kocha huyo sasa ni msaidizi wa Talib Hilal katika
kikosi cha timu ya taifa nya ufukweni ya Oman lakini pia ni kocha wa makipa kwa
timu zote za taifa.
Abeid alifanya vizuri akiwa nchini humo na kikosi
cha Oman Club ambacho ndiyo kikongwe zaidi kama ilivyo kwa Fanja FC.
Coastal Union ipo kambini jijini Muscat na
itajifua kwa wiki mbili katika jiji hilo huku ikicheza mechi za kirafiki
kadhaa.
PICHA: COASTAL UNION SPORTS CLUB







0 COMMENTS:
Post a Comment