Coastal Union imeuanza mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu Bara kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Oljoro.
Pamoja na kuwa nyumbani Mkwakwani, Tanga,
Coastal iliyokuwa kambini nchini Oman ilijikuta ikitoka sare.
Mganda Yayo Lutimba ndiye aliifungia Coastal
Union kabla ya Hamis ‘Maalim’ Saleh kufunga bao la kusawazisha kwa Oljoro
katika dakika ya 88.
0 COMMENTS:
Post a Comment