Azam imeanza Ligi Kuu Bara kwa mwendo wa ‘kusanya pointi
tatu’ baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa bao 1-0.
Katika mechi iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Chamazi,
jijini Dar, bao pekee la wenyeji lilifungwa na Kipre Herman Tchetche.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu, kali na ya kuvutia na kila timu
ilionyesha kupania kupata ushindi.
Hata hivyo, Azam FC watajilaumu kwa kupoteza nafasi kadhaa
ambazo zingeweza kuwapatia mabao zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment