MUSOTI (KULIA) AKIWA NA AYELIKUWA KATIBU MKUU WA SIMBA, EVODIUS MTAWALA NA KAIMU MAKAMU MWENYEKITI, JOSEH ITANG'ARE. |
Beki wa kati wa Simba, Donald Musoti,
amesema alilazimika kuvaa jezi ambayo huvaliwa na kiungo Abdallah Seseme katika
michuano ya Kombe la Mapinduzi kutokana na jezi yake namba tano kusahaulika
jijini Dar.
Musoti, ambaye amekuwa lulu katika safu
ya ulinzi ya Simba, huku akiwa amecheza mechi zote kwenye michuano hiyo
inayofikia tamati leo, aliliambia Championi Jumatatu kuwa, viongozi wa Simba
walimfuata na kumuomba radhi kwa kitendo cha kuisahau jezi hiyo, hivyo kumtaka
avae namba 27 ambayo huvaliwa na Seseme.
“Viongozi walinifuata na kunieleza kuwa jezi
yangu ilisahaulika Dar, wakanipatia hii (27), wakaniambia kuwa nitatumia jezi
hiyo mpaka michuano hiyo itakapomalizika, lakini tukirejea nyumbani nitaendelea
na ileile namba tano,’ alisema Musoti, raia wa Kenya.
Musoti, amekuwa akitumia namba tano,
ambayo ni ya zamani ya Kelvin Yondani ambaye alitimkia Yanga SC, ambako pia
hutumia namba hiyohiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment